Download Video and Audio from YouTube

PART 2: Maisha ya 'MZEE MAJUTO' - Kuzaliwa Hadi Kufa

11,619 views 33 5

PART 2: Maisha ya 'MZEE MAJUTO' - Kuzaliwa Hadi Kufa Amri Athumani, King Majuto alizaliwa mwaka 1948 jijini tanga na kusoma shule ya msambwini, Alianza maisha kwa kujishughulisha na shughuli za kilimo kabla ya kuingia kwenye sanaa ya maigizo ambayo ilimpatia umaarufu mkubwa kijijini kwao na alianza rasmi kuigiza mwaka 1958 akiwa na umri wa miaka 10 na kipindi hicho alikuwa darasa la piliambapo alianza kuigiza katika majukwaa. Mwaka 1966 alimaliza darasa la nane na mwaka uliofuata alijiunga na jeshi la kujenga taifa JKT ambapo alikuwa akilipwa shilingi 20 nakufanya kazi hadi mwaka 1970 alipolazimika kuacha nah ii yote ni kwa sababu ya kupenda kazi ya sanaa ambapo ilikuwa ni ndoto yake tangu alivyokuwa mtoto Na ilipotimu mwaka 1976 kabla ya kujikita kwenye sanaa aliwahi kufanya kazi kwenye kikosi cha zima moto katika kiwanda cha mabalanket na kampuni ya bia Tanzania akiwa mlinzi. Mwaka 1997 mzee king majuto alikutana na biti mmoja mrembo sana aneitwa Aisha Mbwana wakapendana wakaoana mwaka huo huo, na kubarikiwa kuwa na familiya nzuri yenye furaha na watoto. Mzee majuto alibalikiwa kupata watoto 10 aliozaa na bi Asha na wanawake zake wengine ambao kwa bahati mbaya walifariki dunia. Majuto sio jina lake bali ni jina la utani alilopewa na mashabiki zake mwaka 1982 alipojiunga na kundi la DDC kibisa ambapo kazi nyingi alizozifanya zilikuwa za kusikitisha hata kuliza watu na ndipo lilipopatikana jina na king Majuto. mzee majuto maarufu kama king majuto ni mtunzi, muigizaji, mwandishi, na mswada,na ndie muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na akiwa Tanzania film company TFC ambapo alikuwa mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana na maonyesho mbalimbali ya vichekesho vyake ambavyo vilimfanya kushiriki katika sehemu mbalimbali. Install GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Suazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli..